
Beki
wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ amemchambua winga
wa Simba, Shiza Kichuya kwa kusema ni mchezaji wa kawaida na ni rahisi
kumzuia tofauti na wengi wanavyofikiria.
Kauli
hiyo ya Baba Ubaya imekuja baada ya Jumatano wiki hii, Mtibwa Sugar
kutoka suluhu na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Baba
Ubaya amesema kwa beki yeyote anayetumia akili nyingi uwanjani hawezi
kusumbuliwa na Kichuya kwa sababu atakuwa akitumia akili kumdhibiti na
ndiyo maana katika mchezo huo alifanikiwa kumzua asisababishe madhara
langoni kwao.
“Kichuya
ni mchezaji mzuri lakini siyo sana kama wengi wanavyosema au
wanavyodhani kuwa hakabiki, kwangu mimi namuona kuwa ni mchezaji
anayekabika kirahisi sana kama mtu anayemkaba atakuwa anatumia akili na
siyo nguvu kila wakati.
“Amekuwa
akitumia sana mguu wa kushoto tofauti na ule wa kulia, hivyo
ukifanikiwa kumdhibiti asipate nafasi ya kuutumia ipasavyo mguu wake wa
kushoto basi unakuwa umemmaliza.
“Ndiyo
maana amekuwa akipata shida sana kupita upande wangu kila ninapokutana
naye uwanjani (naye anatumia mguu wa kushoto) hata wakati akiwa Mtibwa
kabla ya kujiunga na Simba ilikuwa hivyohivyo,” alisema Baba Ubaya.
0 Maoni:
Post a Comment