Mshambuliaji wa African Sports, Ayoub Lyanga amejiunga na Zanaco ya Zambia.
Lyanga amesajiliwa na timu hiyo kwa mkopo hali ambayo itampa nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lyanga hakuwa mchezaji maarufu sana nchini ingawa imeelezwa kwamba ana uwezo mkubwa wa soka.
Meneja
maarufu katika masuala ya soka nchini, Jamal Kisongo amethibitisha
Mtanzania huyo kupata nafasi ya kuichezea Zanaco akitokea African Sports
inayocheza Ligi Daraja la Kwanza.
“Kweli kabisa kijana Lyanga amejiunga na Zesco ya Zambia kwa mkopo,” alisema Kisongo.
“Naweza kukuambia kama ataendelea kuwa makini na kuendelea kupambana, basi hakuna kinachoweza kumzuia kufanya vizuri.
“Zanaco
ni timu kubwa na inawezekana kabisa itasaidia kumtangaza kama atapata
nafasi lakini huyu kijana ninaamini atakuwa hazina kubwa kwa Tanzania.
Sipendi niseme maneno mengi ila tusubiri,” aliongeza.
Kisongo
ndiye meneja wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta lakini ndiye
meneja wa mshambuliaji mwingine nyota nchini, Thomas Ulimwengu.
0 Maoni:
Post a Comment