ETIHAD
STADIUM Jijini Manchester ndio ndimba la Mechi ya mwisho ya Jumamosi
Januari 21 ya EPL, Ligi Kuu England, kati ya Manchester City na
Tottenham Hotspur, Timu ambazo zipo kikweli kabisa kupigania Ubingwa wa
England.
City, wako Nafasi ya 5 kwenye EPL wakiwa Pointi 3 nyuma ya Timu ya Pili Spurs ambao wako Pointi 7 nyuma ya Vinara Chelsea.
City
wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hali tete baada ya kufungwa Mechi zao
2 kati ya 3 zilizopita na moja ikiwa kisago cha 4-0 toka kwa Everton
kiasi cha kumuacha Meneja wao Pep Guardiola akisalimu amri na kusema
hawana uwezo wa kutwaa Ubingwa.
Spurs, chini
ya Meneja toka Argentina Mauricio Pochettino,tangu wapigwe na Man
United Mwezi Desemba, wameshinda Mechi 6 mfululizo za EPL na kukwea hadi
Nafasi ya Pili.
Hali za Timu.
Man
City sasa wameruhusiwa kumtumia Fowadi Chipukizi hatari wa Brazil
Gabriel Jesus baada Uhamisho wake kukwama kutoka Palmeiras ya Brazil
licha ya kutua kwao kwa Wiki 3 sasa lakini watamkosa Kiungo Fernandinho
ambae yuko Kifungoni.
Spurs watacheza bila ya Beki wao wa kutegemewa Jan Vertonghen ambae sasa imebainika atakuwa nje kwa Wiki 6 baada kuumia Enka.
Walipokutana Uso kwa Uso
- Tottenham wameichapa City Mechi zote 3 zilizopita na ya mwisho ni 2-0 huko White Hart Lane walipoumaliza mwanzo mzuri wa Pep Guardiola kwenye himaya yake mpya na City Msimu huu.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
MAN CITY [Mfumo 4-2-3-1]: Bravo, Sagna, Otamendi, Kolarov, Clichy, Fernando, Toure, Sterling, Silva, De Bruyne, Aguero
TOTTENHAM [Mfumo 3-4-3]: Lloris, Dier, Alderweireld, Davies, Walker, Dembele, Wanyama, Rose, Eriksen, Kane, Alli
Andre Marriner |
0 Maoni:
Post a Comment