Manchester
United watacheza na Stoke City huko Bet365 Stadium leo Jumamosi
wakijua fika kuwa bila ya ushindi ndoto zao za kuwemo kwenye mbio za
Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, zinaweza kuyeyuka.
Wikiendi
iliyopita Man United walitoka Sare 1-1 na Liverpool huko Old Trafford
na kudumisha Rekodi yao ya kutofungwa katika Mechi 16 za Mashindano
yote.
Vile vile, Man United, chini ya Meneja Jose Mourinho, wameshinda Mechi zao 4 za Ugenini zilizopita na 3 zikiwa za EPL.
Hali za Timu
Wakati
Jose Mourinho akiwa na Kikosi kamili cha kuchagua Timu ukimwondoa tu
Eric Bailly ambae yuko huko Gabon kwenye Mashindano ya AFCON 2017 na
Nchi yake Ivory Coast, Meneja wa Stoke City, Mark Hughes, aliewahi
kuichezea Man United Miaka ya nyuma, atawakosa Wachezaji kadhaa akiwemo
Kipa wake Jack na nafasi yake kuchukuliwa na Lee Grant.
Vilevile
Stoke wana Wachezaji Majeruhi ambao ni Geoff Cameron, Stephen Ireland,
Bojan Krkic na Jonathan Walters huku Watatu wakiwa AFCON 2017 na Nchi
zao ambao ni Ramadan Sobhi [Egypt], Mame Biram Diouf [Senegal] na
Wilfried Bony [Ivory Coast].
Fomu ya Stoke
Baada
ya kusuasua, Stoke City hivi karibuni wameanza kupanda Chati na
kushinda Mechi zao zote za EPL kwa Mwaka 2017 kwa kuzifunga Watford,
wakiwa Nyumbani, na Sunderland, Ugenini lakini kati ya hizo wakatupwa
nje ya FA CUP walipofungwa na Wolverhampton Wanderers.
Moja
ya sababu ya ushindi wao kwenye Ligi ni fomu ya Straika wao ‘ngongoti’,
Peter Crouch, ambae amefunga Bao 3 katika Mechi 3 zao za Ligi
zilizopita.
Crouch amebakisha Bao 1 tu kutimiza Bao 100 za Ligi.
Stoke City vs. Manchester United – Mechi zao za hivi karibuni:
Stoke City |
Manchester United |
Sunderland 1-3 Stoke City |
Manchester United 1-1 Liverpool |
Stoke City 0-2 Wolverhamptom |
Manchester United 2-0 Hull City |
Stoke City 2-0 Watford |
Manchester United 4-0 Reading |
Chelsea 4-2 Stoke City |
West Ham United 0-2 Manchester United |
Liverpool 4-1 Stoke City |
Manchester United 2-1 Middlesbrough |
Kwenye Kikosi cha Stoke City, ukimwondoa Meneja wao Mark Hughes, pia wapo Wachezaji kadhaa ambao walianzia Soka lao huko Man United na hao ni Sentahafu Ryan Shawcross na Fulbeki Phil Bardsley na pia Mame Biram Diouf ambae hayupo kwenye Mechi hii.
Mechi ya Mwisho Kukutana
Mechi
ya mwisho kwa Timu hizi kukutana ni huko Old Trafford Mwezi Septemba
walipotoka Sare 1-1 kwa Man United kutangulia kwa Bao la Dakika ya 69 la
Anthony Martial na Stoke kusawazisha Dakika ya 82 kwa Goli la Joe
Allen.
Mechi zilizopita
Hii
itakuwa ni Mechi ya 18 kwa Timu hizi kukutana kwenye EPL na Man United
kushinda Mechi 8 kati ya 9 Jijini Manchester na kupata ugumu huko Stoke
ambako Stoke wameshinda Mechi 2 tu tangu 1984 lakini ushindi huo wa
Mechi hizo 2 ni katika Miaka Mitatu iliyopita.
Mara
ya mwisho kwa Man United kushinda Nyumbani kwa Stoke ni Mwaka 2013
waliposhinda 2-0 Mwezi Aprili wakiwa njiani kutwaa Ubingwa wa England wakiwa chini ya Meneja wao Lejendari Sir Alex Ferguson.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
STOKE CITY [Mfumo 4-2-3-1]: Lee
Grant; Glen Johnson, Erik Pieters, Ryan Shawcross, Bruno Martins Indi;
Charlie Adam, Glenn Whelan; Joe Allen, Marko Arnautovic, Xherdan
Shaqiri; Peter Crouch
MAN UNITED [Mfumo 4-3-3]: David
De Gea; Antonio Valencia, Luke Shaw, Phil Jones, Marcos Rojo; Michael
Carrick, Ander Herrera, Paul Pogba; Anthony Martial, Henrikh Mkhitaryan,
Zlatan Ibrahimovic
Mark Clattenburg |
0 Maoni:
Post a Comment