
Suluhu
waliyoipata Azam, juzi Jumatano dhidi ya Mbeya City, imemfanya kipa wa
Azam, Aishi Manula, kucheza mechi saba mfululizo ambazo ni sawa na
dakika 630 bila ya kuruhusu wavu wake kutikiswa.
Manula
ambaye anasifika kwa uhodari wa kuokoa mikwaju ya penalti, amefanikiwa
kufanya hivyo katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la
Mapinduzi.
Mara
ya mwisho kwake kuruhusu bao ilikuwa ni Desemba 24, mwaka jana kwenye
sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
Baada
ya hapo, akaiongoza Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Prisons, kisha kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi matokeo yalikuwa
hivi; Azam 1-0 Zimamoto, Azam 0-0 Jamhuri, Azam 4-0 Yanga, Azam 1-0
Taifa Jang'ombe na Azam 1-0 Simba.
Manula
anatakiwa kufanya hivyo kwenye mechi nne zijazo ili kuipiku rekodi ya
Muivory Coast, Vincent Angban ambaye kabla ya kuvunjiwa mkataba na
Simba, msimu huu alicheza mechi kumi za kimashindano bila ya kuruhusu
bao.
0 Maoni:
Post a Comment