![]() |
MESSI NA NEYMAR |
UKAME
wa kutoshinda Miaka 9 dhidi ya Real Sociedad wakiwa Uwanjani kwao
Anoeta Stadium ulimalizika Jana Usiku wakati Penati ya Staa wa Brazil
Neymar kuipa Barcelona ushindi wa 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo
Fainali ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme huko Spain.
Penati hiyo ilipigwa Dakika ya 21 baada ya Neymar mwenyewe kuangushwa ndani ya Boksi.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Barca kushinda hapo Anoeta Stadium tangu 2007 na
tangu wakati huo Mechi 11 zishapigwa kati yao hapo hapo Anoeta huku
Barca wakifungwa 5 na Sare 3 katika Mechi 8 zilizopita.
Mara ya mwisho kwa Barca kushinda, Mwaka 2007, Bao za Andrés Iniesta na Samuel Eto’o ndizo ziliwaibua kidedea.
Msimu huu, kwenye La Liga, Real Sociedad na Barca zilitoka 1-1 huko Anoeta Stadium.
Barca
sasa wapo kwenye hatua nzuri ya kutinga Nusu Fainali ya Copa del Rey
ambalo wao ndio Mabingwa Watetezi kwani watarudiana na Real Sociedad
huko Nou Camp Alhamisi ijayo.
Barca wametinga Nusu Fainali za Copa del Rey kwa Misimu 6 mfululizo hadi sasa wakitwaa Kombe mara 3 na mara 2 kufungwa Fainali.
Fainali ya Copa del Rey ni Mei 27.
0 Maoni:
Post a Comment