Raundi ya tano ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam 2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), utaanza Jumamosi Januari 21, 2017 kwa timu za Majimaji na Mighty Elephant za Songea kucheza kwenye Uwanja Majimaji mjini Songea.
Ratiba
ya ASFC inaonesha kwamba timu za Alliance na Mbao za Mwanza zitacheza
pia keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati Young
Africans itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar
es Salaam.
Jumapili
Januari 22, mwaka huu Ruvu Shooting itacheza na Kiluvya United kwenye
Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Toto Africans
itacheza na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza huku Simba itakipiga na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini
Dar es Salaam kadhalika Mbeya Warriors ikicheza na Tanzania Prisons
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Jumatatu
Januari 23, mwaka huu Stand United itacheza na Polisi Mara kwenye
Uwanja wa Karume Mara wakati Azam itacheza na Cosmopolitan kwenye Uwanja
wa Chamazi wakati Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona.
Jumanne
Januari 24, mwaka huu Mtibwa Sugar itacheza na Polisi Moro kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa itacheza na
JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa kucheza na Kabela City
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na Panone zitacheza kwenye
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Januari
25, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na Kagera Sugar
kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mchezo mwingine
utakaozikutanisha timu za African Lyon na Mshikamano utapangiwa tarehe
mpya. Mechi hiyo imepangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru.
IMETOLEWA NA TFF
AZAM SPORTS FEDERATION CUP – RAUNDI YA 5
Ratiba:
Januari 21, 2017
Alliance v Mbao (CCM Kirumba, Mwanza)
Maji Maji v Mighty (Maji Maji, Songea)
Yanga v Ashanti United (Uhuru, Dar es Salaam)
Januari 22, 2017
Ruvu Shooting v Kiluvya United (Mabatini, Mlandizi)
Toto Africans v Mwadui FC (CCM Kirumba, Mwanza)
Simba v Polisi Dar (Uhuru, Dar es Salaam)
Mbeya Warriors v Tanzania Prisons (Sokoine, Mbeya)
Januari 23, 2017
Stand United v Polisi Mara (Karume, Musoma)
Azam FC v Cosmopolitan (Azam Complex, Chamazi)
Ndanda FC v Mlale JKT (Nangwanda Sijaona, Mtwara)
Januari 24, 2016
Mtibwa Sugar v Polisi Moro (Jamhuri, Morogoro)
Kurugenzi FC v JKT Ruvu (Mafinga, Iringa)
Mbeya City v Kabela City (Sokoine, Mbeya)
Madini v Panone (Sheikh Amri Abeid, Arusha)
Januari 25, 2017
Singida United v Kagera Sugar (Namfua, Singida)
Tarehe Kupangwa
African Lyon v Mshikamano (Uhuru, Dar es Salaam)
0 Maoni:
Post a Comment