
SENEGAL
Jana wameichapa Zimbabwe 2-0 katika Mechi ya Kundi B la AFCON 2017,
Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, yanayochezwa
huko Nchini Gabon, na kuwa Nchi ya kwanza kutinga Robo Fainali huku
wakiwa na Mechi 1 mkononi.
Bao
zote za Senegal zilifungwa ndani ya Dakika 13 za kwanza huko Mjini
Franceville, Gabon kupitia Straika wa Liverpool Sadio Mane na Henri
Saivet.
Matokeo hayo, licha ya kuwapeleka Robo Fainali, pia yamehakikisha watamaliza
Kundi B wakiwa ndio Nambari Wani hata wakifungwa na Algeria katika Mechi
yao ya mwisho.
Nao
Tunisia, ambao walichapwa na Senegal 2-0 katika Mechi yao ya kwanza ya
Kundi B, Jana waliifunga Algeria 2-1 katika Mechi nyingine ya Kundi B na
wanahitaji Sare tu na Zimbabwe katika Mechi yao ya mwisho ili waingie
Robo Fainali pamoja na Senegal.
Bao
zote za Mechi ya Tunisia na Algeria zilifungwa Kipindi cha Pili na
Tunisia walifunga Bao lao la kwanza baada ya Krosi ya Youssef Msakni
kutumbukizwa wavuni na Beki wa Algeria Aissa Mandi na la pili kwa Penati
ya Naim Sliti iliyotoloewa baada ya Wahbi Khazri kuchezewa Faulo na
Faouzi Ghoulam.
Algeria walipata Bao lao pekee Dakika za Majeruhi Mfungaji akiwa Sofianne Hanni.
MSIMAMO WA AFCON 2017:
Algeria
sasa wana kibarua kigumu kufuzu Robo Fainali kwani kwanza wanatakiwa
kuifunga Senegal katika Mechi yao ya mwisho na kisha kuomba Zimbabwe
iifunge Algeria na hapo ndipo, pengine, wanaweza kufunga kwa Ubora wa
Magoli au Tombola ya kurushwa Sarafu.
Leo zipo Mechi 2 za Kundi C kati ya Mabingwa Watetezi Ivory Coast na Congo DR na nyingine ni Morocco na Togo.
0 Maoni:
Post a Comment