
MANCHESTER
City sasa wameruhusiwa kumtumia Staa Mbrazil wa Miaka 19 Gabriel Jesus
kwenye Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, ya Jumamosi dhidi ya
Tottenham Hotspur.
City
walishafikia makubaliano na Klabu ya Brazil Palmeiras tangu Mwezi Julai
Mwaka Jana kumnunua Kinda huyo wa Brazil mwenye Miaka 19 kwa Dau la
Pauni Milioni 27 na pia kukubali Mchezaji huyo abakie Palmeiras hadi
Msimu wa Brazil utakapoisha Mwezi Desemba.
Jesus
amekuwa Kambini na City kwa Wiki 3 sasa lakini ukiritimba umekwamisha
Uhamisho wake kukamilika rasmi na hivyo kusitisha kuichezea rasmi City.
Kinda
huyo ndio kwanza amechomoza kwenye Soka la Dunia akiwa na Msimu wa Pili
tu na Palmeiras lakini akaiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Taifa
Mwezi Novemba baada ya kutwaa Medali ya Dhahabu akiichezea Brazil kwenye
Michezo ya Olimpiki, RIO 2016, Mwezi Julai.
JUA KIDOGO KUHUSU GABRIEL JESUS.
- Jesus alijilukana kama Gabriel Fernando alipoanza kuichezea Palmeiras akiwa na Miaka 17.
- Akiwa huko alipewa Jezi Namba 33 [Umri wa Yesu Kristu] na mmoja wa Maafisa Habari wa Klabu hiyo akamwambia atumie Jina la Gabriel Jesus.
- Akiwa na Man City, Jesus pia atavaa Jezi Namba 33 ambayo awali ilivaliwa na Nahodha wa City Vincent Kompany.
Jesus
alianza kukichezea Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Taifa ya Brazil Mwezi
Septemba Mwaka Jana na kufunga Bao 4 katika Mechi zake 6.
Hivi
sasa Man City wapo Nafasi ya 5 kwenye EPL, wakiwa Pointi 10, nyuma ya
Vinara Chelsea baada ya kufungwa Mechi 2 kati ya 3 walizocheza mwisho.
******************************************************************
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
++Saa kwa mujibu wa saa za Bongo++
Jumamosi Januari 21
1530 Liverpool v Swansea City
1800 Bournemouth v Watford
1800 Crystal Palace v Everton
1800 Middlesbrough v West Ham United
1800 Stoke City v Manchester United
1800 West Bromwich Albion v Sunderland
2030 Manchester City v Tottenham Hotspur
Jumapili Januari 22
1500 Southampton v Leicester City
1715 Arsenal v Burnley
1930 Chelsea v Hull City
0 Maoni:
Post a Comment