Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, hali ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa,
imeendelea kuwa mbaya baada ya majani ya uwanja huo kukauka kutokana na
idara ya maji safi na maji taka kukata huduma ya maji katika uwanja huo
kutokana na deni wanalodaiwa wamiliki wake.
Meneja
wa uwanja huo, Steven Shija, amenukuliwa akisema: "Ni kweli uwanja hali
yake siyo nzuri, hii inatokana na idara ya maji kukata maji hapa
uwanjani, hivyo tukakosa namna ya kuumwagilia lakini tumeshalipa deni
tulilokuwa tunadaiwa na sasa tutaanza kuumwagilia ili urudi katika hali
yake kama zamani.
"Baada
ya kulipa deni, kuna kifaa kitaletwa kwa ajili ya kuruhusu maji kuingia
ndani na yakishaingia tutaumwagilia uwanja huu usiku na mchana ili
haraka uweze kurudi katika hadhi yake.”
SOURCE: CHAMPIONI
0 Maoni:
Post a Comment