Hii
imezoeleka mpambano kati ya timu hasimu za Simba na Yanga zinapokutana
kunakuwa na vitendo vya kishirikina vinakuwa vinafanywa uwanjani lakini
kwenye mechi ya jana baina ya timu hizo visiwani Zanzibar hakukuwepo na
vitendo hivyo.
Unajua
ilikuaje soma hapa:
uwanjawa Amaan ulipofanyika mchezo huo umekuwa
ukitumiwa na jeshi la Zanzibar kwa ajili ya kufanyia mazoezi kuanzia
asubuhi hadi alasiri kwa ajili ya kujiandaa na sherehe za Mapinduzi
ambazo zitafanyika kesho Alhamisi.
Pale uwanjani
hapo liliwashuhudia makomandoo wa timu hizo wakiwa wanahaha kuzama
ndani na kufanya mambo yao lakini wanajeshi waliokuwa wanafanya mazoezi
uwanjani hapo hawakuruhusu mtu yeyote asiye mwana usalama kuingia ndani
ya uwanja huo hadi saa tisa walipoziruhusu timu za Taifa ya Jang’ombe na
Azam.
Kutokana
na hali hiyo makomandoo hao walilazimika kukaa nje na juhudi zao za
kutaka kufanya vitendo vya kishirikina vikakwama huku wengine
wakionakana kuwasiliana kwa simu mara kwa mara.
0 Maoni:
Post a Comment