Aliyekuwa
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa amemtaja
mshambuliaji wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo kuwa
ndiye aliyemchagua kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka 2016.
Tuzo hizo zilitolewa juzi nchini Uswisi ambapo Ronaldo aliwashinda Lionel Messi na Antonio Griezmann.
Ronaldo, mwishoni mwa mwaka jana, alifanikiwa kuwashinda Messi na Griezmann na kubeba Tuzo ya Ballon d’Or.
Mkwasa
amesema "alikuwa ana kila sababu ya kumchagua Ronaldo kushinda tuzo hiyo
kutokana na msaada mkubwa ambao aliutoa kwenye klabu yake ya Real
Madrid na Ureno".
Mkwasa
alisema, sababu ya kwanza iliyomshawishi kumpa kura yake Ronaldo ni
kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kubeba Ubingwa wa Ulaya, pia
aliisaidia Ureno kubeba Ubingwa wa Euro nchini Ufaransa.
“Tofauti
na sifa zote alizokuwa nazo Ronaldo ikiwemo ya kuisaidia klabu yake ya
Real Madrid kubeba Ubingwa wa Ulaya, pia kuisaidia timu yake ya taifa ya
Ureno kubeba Ubingwa wa Ulaya kwenye euro 2016 nchini Ufaransa,
navutiwa na nidhamu yake ndani na nje ya uwanja.
“Hizo ndiyo sifa kubwa alizokuwa nazo Ronaldo zilizonishawishi mimi nimpe kura yangu,”alisema Mkwasa.
Aidha,
kwa upande wa makocha Mkwasa alimpigia kura ya kwanza Kocha Mkuu wa
Liverpool, Jurgen Klopp, ya pili akampa Kocha Mkuu wa Manchester City,
Pep Guardiola na ya tatu ilienda kwa Kocha Mkuu wa Real Madrid, Zinedine
Zidane.
Kwa
upande wa Nahodha Mkuu wa Taifa Stars, Mbwana Samatta yeye alimpa kura
ya kwanza Kocha Mkuu wa Barcelona, Luis Enrique, ya pili akampa,
Guardiola na tatu ikaenda kwa kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone.
0 Maoni:
Post a Comment