Mwanamiereka wa WWE,Jimmy Snuka alimaarufu kama 'Superfly' amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Wakili wake amesema mwanamiereka huyo aliaga dunia akiwa katika nyumba ya mkwe wake mjini Florida, akiwa pamoja na familia yake.
Mzaliwa
huyo wa Fiji alikuwa wakati mwingi hospitalini kwa shida tofauti
ikiwemo ugonjwa wa kiakili wa Dementia, lakini chanzo cha kifo chake
bado hakijabainika
Katika taarifa kwenye mtandao wa shirika la WWE
imesema imesikitishwa na kifo kilichompata 'mwanzilishi wa kitengo cha
high flying' katika ukumbi wamiereka.
Mtoto wake Tamina Snuka,
pia nyota wa miereka, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, 'Nakupenda
babangu' na kuambatisha picha yake na babake kwenye ujumbe wake huo.

Ni chini ya wiki mbili tangu, mashtaka ya mauaji kutupiliwa mbali dhidi yake kuhusiana na kifo cha mpenzi wake mwaka 1983.
Jaji
alitoa uamuzi huo baada ya kubaini Jimmy alikuwa na upungufu wa kiakili
na hangeweza kuendelea na kesi hiyo ya mauaji ya mpenzi wake Nancy
Argentino.
Mashtaka hayo waliwasilishwa mahakamani mwaka 2015.
Alikana madai hayo ya mauaji. Nyota wa miereka wamekuwa wakituma risala za rambirambi kwa Snuka kwenye mitandao ya kijamii.
0 Maoni:
Post a Comment