Straika
nyota wa Yanga, Amissi Tambwe, amebakiza miezi minne amalize mkataba
wake wa kuitumikia klabu hiyo ambayo alijiunga nayo msimu wa 2014/15
akitokea Simba.
Hata
hivyo, Tambwe kabla ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga wa
kuongeza mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, hivi
karibuni amepokea ofa kwenda kujiunga na timu moja inayoshiriki ligi kuu
ya nchini Algeria.
Tambwe
amesema kuwa ofa hiyo ameipata kupitia kwa wakala wake lakini
ameshindwa kufanya maamuzi mpaka hapo atakapoiona ofa atakayopewa na
klabu yake ya sasa ya Yanga ambayo pia ilimuahidi kumpatia dau zuri
baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
“Bado
sijafanya mazungumzo yoyote yale na uongozi kuhusiana na mkataba mpya
lakini kuhusu kufanya mazungumzo na timu za nje hilo ni kweli, kuna timu
moja inanitaka hata viongozi wa Yanga wanalijua hilo.
“Viongozi
wa timu hiyo kutoka Algeria waliwahi kuja siku chache baada ya dirisha
dogo la usajili kufungwa na walipowaambia viongozi wangu wanisajili
lakini nitajiunga nao baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi kuu
walikataa, hivyo kwa sasa wamekuja tena ila bado sijawakubalia mpaka
nitakapopata ofa ya Yanga,” alisema Tambwe huku akikataa kuitaja timu
hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment