WACHEZAJI WA WEST HAM WALIMTAKA DIMITRI PAYET AONDOKE.

Tokeo la picha la PAYET IMAGE

Wachezaji wa klabu ya West Ham walitaka Dimitri Payet kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuelekea Mersaille kulingana na mwenyekiti mwenza wa klabu hiyo David Sullivan.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 alijiunga tena na klabu yake ya zamani kwa kitita cha pauni milioni 25 baada ya kudaiwa kukataa kuichezea West Ham kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Tokeo la picha la DAVID SULLIVAN IMAGE

''Kwa kweli hatukutaka aondoke lakini huwezi kwenda kinyume na umoja wa timu'' ,sullivan aliambia BBC.

Sullivan alisema kuwa Payet aliamua kutochukua mshahara wake wa Januari.

''Payet hakuzungumza na mtu kwa wiki sita. Amekataa kuzungumza na mtu yeyote katika timu'', alisema Sullivan.

Payet alijiunga na West Ham mwezi Juni 2015.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment