Mara ya mwisho Watford kuifunga Arsenal katika uwanja wake wa nyumbani ilikuwa 1988 |
Matumaini ya klabu ya Arsenal kutwaa ubingwa wa England yanaanza kufifia baada ya kuchapwa na Watford 2-1 na hii ni Emirates.
Mlinzi
wa zamani wa Tottenham Younes Kaboul alianza kuiandikia Watford goli la
kwanza dakika ya 10 baada ya kuachia shuti kali lililomgonga Aaron
Ramsey na kutinga nyavuni.
Dakika mbili na sekunde 57 baadaye Troy
Deeney akaiandikia goli la pili Watford baada ya mpira uliopigwa na
Etienne Capoue kupanguliwa na mlinda mlango Peter Cech na kisha kumkuta
Troy aliyendika bao safi.
Kipindi cha pili Arsenal walianza kwa
kasi na kujipatia goli la kufutia machozi kutoka kwa Alex Iwobi baada ya
kupata pande safi lililochongwa na Alexis Sanchez.
Kwa mara ya
mwisho Arsenal kushinda kikombe cha ligi kuu England ilikuwa msimu wa
mwaka 2003-04 na kwa sasa wapo nyuma kwa alama tisa dhidi ya vinara
Chelsea ambao wametoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Liverpool.
0 Maoni:
Post a Comment