YANGA YAMTANGAZA RASMI MKWASA KATIKA NAFASI YA KATIBU MKUU

Tokeo la picha la MKWASA IMAGE
 
Taarifa kutoka Yanga zinasema kuwa kuanzia sasa aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa ametangazwa kuwa Katibu Mkuu wa Yanga rasmi.
Kabla ya Mkwasa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania alikuwa kocha msaidizi wa Yanga chini ya kocha mkuu wakati huo Hans van Pluijm.

Mkwasa aliachana na Taifa Stars mwezi huu na Taifa Stars kuingia mkataba wa muda mfupi na Salum Mayanga wakitarajia kumuongeza mkataba au kutafuta kocha mwingine.

Mkwasa kwa sasa hana timu na yupo katika mapumziko yake binafsi kwa hiyo huenda akajiunga na Yanga kama katibu mkuu na kuongeza nguvu katika klabu hiyo ili kuweza kuchukua taji la ligi kuu msimu huu lakini pia kuisaidia kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika.

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment