Shirikisho la soka Ulimwenguni (FIFA) hapo jana limetoa orodha mpya ya ubora wa viwango vya soka Duniani kwa nchi Wanachama , na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia Brazil na kwa Afrika ni Misri ndio wapo juu kabisa huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.
5
Bora kwenye orodha hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko na nazo ni
Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).
Kwa
Afrika, Nchi ambayo iko juu kabisa ni Misri, waliotolewa Fainali ya
AFCON 2017, ambao sasa wapo Nafasi ya 23 baada ya kupanda Nafasi 12
wakifuatiwa na Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao
ni Cameroon, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29.
Orodha hiyo ni;
- Argentina
- Brazil
- Germany
- Chile
- Belgium
- France
- Colombia
- Portugal
- Uruguay
- Spain
- Switzerland
- Wales
- England
- Poland
- Italy
- Croatia
- Mexico
- Peru
- Costa Rica
- Iceland
Kwa upande wa Afrika Uganda bado wanaendelea kuongoza kwa
Afrika Mashariki wakiwa nafasi ya 17 kwa Afrika na 75 duniani
wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 20 Afrika na 87 duniani wakati
Rwanda wako nafasi ya 27 Afrika na 100 duniani na Burundi nafasi ya 40
Afrika na 138 duniani.
Kwa upande wa Afrika Misri wamekuwa vinara
kwa kukwea kwa nafasi 12 na kutua kileleni wakiwa nafasi ya 23,
wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 31 huku mabingwa wa michuano ya
Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi 29 mpaka nafasi ya
33 duniani.
0 Maoni:
Post a Comment