Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez amedai kuwa ana
matumaini ya kwamba rufani yake itakayokatwa itaweza kumuokoa asikose
mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu
katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili dhidi ya Atletico
Madrid.
Suarez aliifungia Barcelona bao katika mchezo ambao
ulishuhudia wachezaji watatu wakipewa kadi nyekundu katika sare ya bao
1-1 iliyofanya Barcelona kufuzu fainali ya nne mfululizo kwa jumla
ya mabao 3-2.
Hata hivyo nyota huyo wa kimataifa wa Argentina
alitolewa nje kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa
Barcelona baada ya mwamuzi kudhani alimpiga kiwiko Koke katika dakika
za majeruhi.
Suarez amesema kadi hiyo aliyopewa inamfanya ajisikie
kucheka kwani inaonekana kama mwamuzi alidhamiria kufanya hivyo. Suarez
aliendelea kudai kuwa wanataka kuona kama wanaweza kukata rufani
kwasababu hadhani kama alifanya kosa lolote kustahili adhabu hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment