NDONDI: MOHAMED MATUMLA NJE YA ULINGO.

Tokeo la picha la mohamed matumla image

Hatimaye bondia wa Tanzania Mohammed Matumla ametakiwa kupumzika kwa muda wa miezi 10 hadi 12 kufuatia kupigwa kwa Knockout (KO) na kupata maumivu makali ya kichwa na mpinzani wake bondia Mfaume Mfaume na kupelekea kufanyiwa upasuaji katika pambano lisilo la ubingwa.

Matumla alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya raundi 10 na ya mwisho kupigwa KO mbaya kufuatia kusukumiwa makonde mazito na mpinzani wake.

Mtoto huyo wa bondia gwiji wa zamani nchini, Rashid Matumla alifikishwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Muhimbili, kabla ya kutolewa na kuwekwa wadi ya kawaida.

Kwa sasa mwana ndinga huyo anaendeea vizuri huku akiendelea kupatiwa matibabu katika hospaitali ya taifa ya muhimbili jijini Dar es salaam chini ya uangalizi mkubwa wa madaktari.

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment