Arsenal "walisambaratika kiakili" wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya hatua ya 16 bora mikononi mwa Bayern Munich, meneja Arsene
Wenger amesema.
"Ni vigumu kueleza," Wenger aliambia BT Sport.
"Muda mfupi kabla ya mapumziko, tulikuwa na nafasi mbili nzuri za kufunga. Tulirejea na kucheza vyema.
"Kipindi
cha pili, tulimpoteza Koscielny upesi - alitoka tukiwa 1-1 - na
hatimaye tukasambaratika. Bayern ni timu nzuri kutushinda vpia.
"Nilihisi bao la tatu liliangamiza wachezaji wetu kabisa kwa sababu baada ya hapo hatukuweza kujibu tena.
Arjen Robben aliwaweka Bayern mbele, lakini Arsenal wakasawazisha
kupitia Alexis Sanchez aliyefuatilia penalti yake ambayo ilikuwa
imekombolewa na kipa.
Kipindi cha pili, Gunners waliporomoka,
Bayern walitamba kwa dakika 10 ambapo Robert Lewandowski alirejesha
uongozi wa Bayern kabla ya Thiago Alcantara kufunga mabao mengine
mawili.
Nguvu mpya Thomas Muller alifunga bao dakika za mwishomwisho.
Alipoulizwa iwapo Arsenal wanahitaji "muujiza", Wenger alijibu: "Bila shaka".
Mfaransa
huyo alijibu maswali matatu pekee katika kikao chake na wanahabari
baada ya mechi, ambacho kilidumu chini ya dakika tatu.
0 Maoni:
Post a Comment