REFA CLATTENBURG AIMWAGA LIGI KUU ENGLAND KWENDA SAUDIA

Tokeo la picha la Mark Clattenburg image

Mark Clattenburg ameacha kuwa Refa wa EPL, Ligi Kuu England, baada ya kupata wadhifa mwingine huko Nchini Saudi Arabia.
 
PGMOL, Professional Game Match Officials Limited, Taasisi ya Marefa huko England imetamka Refa huyo mwenye Miaka 41 amepata kazi huko Shirikisho la Soka la Saudi Arabia.

Clattenburg, ambae ndie aliendesha Fainali za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, FA CUP na EURO 2016, Msimu uliopita, aliwasilisha ombi lake la kung’atuka toka PGMOL tangu Desemba.

Clattenburg aliwekwa kwenye Listi spesheli ya Marefa wa PGMOL wanaochezesha EPL tu tangu 2004 na kutumikia kwa Miaka 12 kwenye Ligi hiyo.

Lakini, Mwaka 2008 na 2009, aliwahi kufungiwa Miezi 8 baada ya PGMOL kugundua kuna hitilafu kuhusu kazi zake nje ya Urefa.

Mwaka 2012, Chelsea iliwahi kumshitaki kwa kuwa Mbaguzi dhidi ya Mchezaji wao kutoka Nigeria Jon Obi Mikel wakati wa Mechi na Manchester United lakini alisafishwa tuhuma hizo.

Mwaka 2014, Clattenburg alipewa onyo na Mkuu wa PGMOL Mike Riley kwa kukiuka Maadili ya Kirefa kwa kuongea kwa Simu na Meneja wa Crystal Palace mara baada ya Mechi kati ya Palace na West Brom na pia kuondoka Uwanjani kutoka kwenye Mechi hiyo bila kuambatana na Marefa wenzake kinyume na taratibu za Marefa chini ya PGMOL.

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment