UEFA EUROPA RAUNDI YA MTOANO: ZLATAN IBRAHIMOVIC HATITRIKI, MAN UNITED SAFI.

 Tokeo la picha la man u vs st etiene image

Manchester United wakiwa kwao Old Trafford wameitwanga St-Etienne ya France 3-0 kwa Hatitriki ya Zlatan Ibrahimovic katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
 
Bao hizo ziliendeleza Rekodi ya Zlatan Ibrahimovic ya kuibamiza St-Etienne kila akikutana nayo Rekodi ambayo aliiweka akiwa na Paris St-Germain ambako alifunga Bao 14 katika Mechi 13 dhidi yao. 

Mvuto mwingine wa Mechi hii ni kupambanishwa kwa Mtu na Kaka yake Paul Pogba wa Man United na Kaka Mkubwa Florentin Pogba Beki wa St-Etienne ambae hakudumu Dakika 90 baada ya kuumia Dakika ya 79 na kubadilishwa huku Mdogo Mtu akikosa Bao kadhaa na kupiga Posti pia.

 Tokeo la picha la man u vs st etiene image

Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 15 kwa Frikiki ya Zlatan Ibrahimovic iliyombabatiza Mchezaji wa St-Etienne Pajot na kutinga. Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.

Kipindi cha Pili Zlatan Ibrahimovic alifunga Bao nyingine 2 katika Dakika za 75 baada ya kazi njema ya Marcus Rashford na jingine Penati ya Dakika ya 88 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye boksi.
 Tokeo la picha la man u vs st etiene image

Timu nyingine ya England ambayo iko EUROPA LIGI ni Tottenham ambayo ilifungwa 1-0 na Klabu ya Belgium Gent.
Nayo Klabu ya Straika wa Tanzania, Mbwana Samatta, Genk ya Belgium imetoka Sare 2-2 na Astra Giurgiu ya Romania kwenye Mechi iliyochezwa huko Nchini Romania na Wenyeji hao kunusurika kipigo kwa kusawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la Takayuki Seto.

Kwenye Mechi hiyo, ambayo Samatta alicheza Dakika zote 90, Genk walitangulia kufunga Dakika ya 25 kwa Bao la Timoty Castagne 25 na Astra kusawazisha Dakika ya 43 kwa Goli la Constantin Budescu 43.

Leandro Trossard, Dakika ya 83, aliipa Genk Bao la Pili.
Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zitachezwa Alhamisi Februari 23.

VIKOSI:
Manchester United: Romero, Valencia, Smalling, Bailly, Blind, Mata [Rashford, 69’], Herrera, Fellaini [Lingard 45'], Martial [Young, 84’], Pogba, Ibrahimovic.
Akiba: de Gea, Rojo, Lingard, Young, Rashford, Schweinsteiger, Darmian.

Saint-Étienne: Ruffier, Malcuit, Perrin, Theophile-Catherine, Pogba [Beric, 79’], Jorginho, Veretout, Pajot [Selnaes, 70’], Monnet-Paquet [Roux 65'], Saivet, Hamouma.
Akiba: Moulin, Lacroix, Roux, Selnaes, Lemoine, Beric, Pierre Gabriel.
 Tokeo la picha la Pavel Královec IMAGE
             REFA: Pavel Královec (Czech Republic)


UEFA EUROPA LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Mechi za Kwanza
Matokeo:

Krasnodar 1 Fenerbahce 0
AZ Alkmaar 1 Lyon 0
Celta Vigo 0 Shakhtar Donetsk 1
Borussia Monchengladbach 0 Fiorentina 1
Olympiakos 0 Osmanlispor 0
KAA Gent 1 Tottenham Hotspur 1
FK Rostov 4 Sparta Prague 0
Astra Giurgiu 2 Genk 2
Ludogorets 1 FC Copenhagen 2
Athletic Bilbao 3 Apoel Nicosia 2
Legia Warsaw 0 Ajax 0
Anderlecht 2 Zenit St Petersburg 0
Manchester United 3 Saint-Etienne 0
Villarreal 0 AS Roma 4
Hapoel Beer Sheva 1 Besiktas 3
PAOK 0 Schalke 3
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment