KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Geoffrey Bonny
Namwandu (37) amefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kusumbuliwa na
maradhi kwa muda mrefu.
Dada
wa mchezaji huyo wa zamani wa Prisons ya Mbeya na Yanga SC ya Dar es Salaam,
Neema ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online jana kwamba wamempoteza kipenzi chao
baada ya kuhangaika naye kumuuguza kwa muda mrefu.
Neema
amesema kwamba msiba upo nyumbani kwao mjini Mbeya ambako taratibu za mazishi
zimekwishaanza.
Bonny alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars enzi za kocha Mbrazil, Marcio Maximo na wengi wanamkumbuka kwa soka
yake maridadi katika sehemu ya kiungo, licha ya kwamba aliibuliwa wakati umri
wake umekwishaenda.
Alicheza
Yanga chini ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Kondic na akaendelea hata
alipoondolewa mwalimu huyo na kuletwa Mseribia mwingine, Kostadin Papic.
Ni kati ya wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kukata
tiketi ya kucheza fainali pekee za michauno ya Ubingwa wa Afrika (CHAN)
zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Hata
hivyo, Maximo akamtema katika kikosi cha Stars baada ya fainali za CHAN nchini
Ivory Coast mwaka 2009 kutokana na kuwa majeruhi.
Maumivu
hayo yalimfanya aachwe na Yanga mwaka 2011 akaenda kumalizia soka yake
Simrik SYC ya Nepal.
MWENYEZI MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI
Simrik SYC ya Nepal.
MWENYEZI MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI
0 Maoni:
Post a Comment