CLAUDIO
Ranieri, Meneja alieipa Leicester City Ubingwa wao wa kwanza katika
Historia yao na kufukuzwa kazi baada ya Miezi 9 tu, Leo ametoa
tamko ambalo limechoma Mioyo ya wengi.
Alianza: ‘Jana Ndoto yangu ilikufa!’
AWALI:
MABINGWA wa England LeicesterCity wamemfukuza kazi Meneja wao ikiwa ni Miezi 9 tu baada ya kuwapa, bila kutegemewa, Ubingwa wao wa kwanza wa England katika Historia yao.
Habari
hizi zimetolewa na Bodi ya Leicester City na zimekuja Siku 1 tu baada
ya Klabu hiyo kufungwa 2-1 huko Spain na Sevilla katika Mechi yao ya
kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Ranieri,
mwenye Miaka 65, aliiongoza Leicester, kwa mshangao wa wengi, kutwaa
Ubingwa wa England Msimu uliopita wakiwa mbele kwa Pointi 10 lakini
Msimu huu mambo yako mrama na wako hatarini kuporomoka Daraja.
Likitokea hilo basi wao ndio watakuwa Mabingwa Watetezi wa kwanza wa England kushuka Daraja tangu 1938.
Leicester
wamepoteza Mechi zao 5 za Ligi zilizopita na ndio Klabu pekee katika
Madaraja yote Manne ya England ambayo haijafunga hata Bao 1 la Ligi
Mwaka huu 2017.
Mechi ijayo kwa Leicester ni kwao King Power Stadium Jumatatu ijayo dhidi ya Liverpool.
0 Maoni:
Post a Comment