CAMEROON
Jana huko Libreville, Gabon, walitoka nyuma kwa Bao 1 na kuibwaga Egypt
2-1 na kutwaa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika katika Mashindano ya 31 ya
AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Cameroun kuifunga Egypt katika Fainali 3
walizokutana nayo huko nyuma na hii ni mara yao ya kwanza kutwaa Ubingwa
wa Afrika tangu Mwaka 2002 ilipokuwa mara yao ya 4 kuwa Bingwa.
Egypt
ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 22 Mfungaji akiwa Kiungo wa
Arsenal Mohamed Elneny na Bao hilo kudumu hadi Haf-taimu.
Kipindi
cha Pili, Wachezaji Wawili wa Cameroon walioanzia Benchi ndio waligeuza
Mechi pale Nicolas N’Koulou aliposawazisha Dakika ya 59 na Vincent
Aboubakar kuwapa ushindi Dakika ya 88.
Bao hizo ziliamsha nderemo na vifijo miongoni mwa Mashabiki 38,000 wengi wao wakiwa ni wa Cameroon.
VIKOSI:
EGYPT:
Essam El Hadary, Ahmed Fathi, Ahmed Hegazy, Ali Gabr, Ahmed Elmohamady,
Mohamed Elneny, Tarek Hamed, Amr Warda, Abdallah Said, Mahmoud Hassan
(Ramadan Sobhi 66’), Mohamed Salah
CAMEROON:
Fabrice Ondoua, Michael Ngadeu-Ngadjui, Collins Fai, Adolphe Teikeu
(Nicolas N’Koulou 32’), Ambroise Oyongo, Sébastien Siani, Arnaud
Sutchuin Djoum, Benjamin Moukandjo, Robert Ndip Tambe (Vincent Aboubakar
46’), Christian Bassogog, Jacques Zoua (Georges Mandjeck 90+4’)
0 Maoni:
Post a Comment