Kiungo
wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain amewaomba radhi Wanaarsenal baada
ya “kulaiki” post iliyokuwa ikisisitiza “Wenger aende zake”.
Mashabiki
wa Arsenal Fan TV waliweka post hiyo wakionyesha kuchoshwa na Kocha
Arsene Wenger wakimtaka aende baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa
Chelsea.
Baada ya hapo Oxlade-Chamberlain alionekana akiwa “amelaiki” kama sehemu ya kuunga mono.
Lakini baadaye alitupia mtandaoni akiomba radhi kwamba hakumaanisha na wala hakuwa na nia ya kufanya hivyo.
0 Maoni:
Post a Comment