Ligi kuu ya soka ya
Tanzania bara siku ya jana iliendelea kwa michezo kadhaa huku wengi
wakiitupia macho mechi ya Majimaji dhidi ya Simba mjini Songea katika
mchezo uliokuwa unaumuhimu kwa pande zote mbili.
Katika kuonyesha kitu
kinachoitwa kutokata tamaa Simba jana wameiadabisha Majimaji ya Songea
Bao 3-0 huku nyota ambao walikuwa hawapewi nafasi ya kuanza mara kwa
mara katika kikosi hicho wakiongoza mauaji.
Mshambuliaji Ibrahim
Ajib migomba ndie alikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za majimaji kabla
ya kiungo Said hamis Ndemla kuweka msumari wa pili na kupoteza matumaini
ya majimaji.
Laudit Mavugo alishindilia msumari wa tatu na kuzidi kudidimiza ndoto za majimaji kubaki ligi kuu msimu huu.
Huu ni ushindi mkubwa kuupata Simba katika mwaka 2017 tangu warudi kwenye VPL'
0 Maoni:
Post a Comment