JUMAMOSI Februari 25, Barabara na vichochoro vyote vitaelekea Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kushuhudia mtanange kati ya Vigogo Wawili Nchini, Simba na Yanga, wakipambana kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom.
Mbali ya hii kuwa Dabi, kihalali inapaswa kuitwa Dabi ya Kariakoo kutokana na ukweli Timu zote ni za Kitongoji cha Kariakoo Jijini Dar, Mechi hii inakutanisha Mahasimu hawa wakiwa wao Wawili ndio pekee wamo kwenye mbio kali na halisi za Ubingwa wa Tanzania Bara Msimu huu.
VPL, inayoshirikisha Timu 16, sasa inaongozwa na Simba wenye Pointi 51 kwa Mechi 22 na Yanga ni wa Pili wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 21 huku Azam FC ni wa 3 wakiwa na Pointi 41 kwa Mechi 23.
Simba, chini ya Kocha kutoka Cameroun, Joseph Omog, akisaidiwa na Mganda Jackson Mayanja, wamepiga Kambi huko Zanzibar wakati Yanga, chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina, anaesaidiwa na Juma Mwambusi, wako huko Kigamboni, eneo la Kimbiji, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.
Kambi zote mbili zimekuwa ‘bubu’ kuzungumzia hali halisi za Vikosi vyao, hususani Wachezaji walioripotiwa Majeruhi, na zote zimesisitiza umuhimu wa Bigi Mechi hii na kujipa moyo wa ushindi.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM
VIINGILIO:
- VIP A 30000
- VIP B NA C 20,000
- ORANGE 10,000
- KIJANI NA BLUE 7000
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Mbali ya Timu husika kuhaha kwa matayarisho ya mtanange huu, Washabiki pia wamekuwa kwenye pilikapilika za kununua Tiketi mapema kupitia MaxMalipo lakini ripoti zimezagaa kuwa Tiketi hizo zimeanza kuadimika baada ya kununuliwa kwa wingi mapema mno.
Tiketi ambazo zimedaiwa kuadimika mno ni zile za Bei ya chini, Shilingi 7,000 na 10,000, na ipo dhana zitaibuka mikononi mwa Watu baki leo Ijumaa na Siku ya Mechi Jumamosi zikiuzwa kwa Bei ya juu.
0 Maoni:
Post a Comment