ROONEY AMESEMA ANABAKI OLD TRAFFORD.

  Tokeo la picha la rooney images
KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney ametoa Taarifa rasmi kukanusha kuwa yuko mbioni kuhamia China kabla Dirisha la Uhamisho la Nchi hiyo halijafungwa Jumanne ijayo Februari 28.

Habari za kuhama kwa Rooney zilishika hatamu mara baada ya kuripotiwa kuwa Wakala wake, Paul Stretford, yuko huko China kukamilisha Dili ya Uhamisho.

Leo hii, Rooney, mwenye Miaka 31 na ambae Mkataba wake na Man United unamalizika 2019, amesisitiza yupo na atabaki Man United kwenye Vita yao ya Mstari wa Mbele kwenye Mashindano Manne.

Jumapili Man United wako huko Wembley Jijini London kucheza Fainali ya Kombe la Ligi, EFL CUP, na Southampton, na pia wamefuzu kutinga Robo Fainali ya FA CUP huku pia Jana wakifanikiwa kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI wakati pia kwenye EPL, Ligi Kuu England, bado wamo mno kwenye kinyang’anyiro cha kutinga 4 Bora.

TAMKO LA ROONEY:
“Ingawa Klabu kadhaa zimeonyesha nia, ambapo nashkuru, mie nataka kumaliza haya na kusema nabakia Manchester United. Natumaini nitashiriki kikamilifu kuisaidia Timu kufanikiwa katika vita yake ya pande 4! Ni wakati wa kufurahisha kwa Klabu na nataka niwe moja ya sehemu yake!”

Nyuma ya Pazia
Hivi sasa Rooney hana namba kwenye Kikosi cha Kwanza cha Man United na hajacheza tangu Februari 1 akidaiwa kuwa na maumivu ya Misuli.

Wiki hii Rooney alirejea Mazoezini lakini hakujumuika kwenye Kikosi kilichoenda France ambacho Juzi kiliifunga Saint-Etienne 1-0 na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.

Jumapili Man United wapo huko Wembley Jijini London kucheza Fainali ya Kombe la Ligi, EFL CUP, dhidi ya Southampton na hadi sasa hamna uhakika kama Rooney atakuwemo miongoni ma Wachezaji kwa ajili ya Mechi hiyo.

Inaaminika kuwa chaguo la Rooney ni kubakia Man United hadi 2019 ambapo Mkataba wake utamalizika ili apate fursa kuichezea Timu ya Taifa ya England Mechi 7 zaidi ili aweke Rekodi ya kuwa ndie Mchezaji alieichezea Nchi hiyo Mechi nyingi zaidi katika Historia yake.

Akiwa na Man United, Rooney ametwaa Ubingwa wa England mara 5 na UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 1 tangu ajiunge nao Mwaka 2004 akiwa na Miaka 18 kutoka Everton kwa Dau la Pauni Milioni 27.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment