Mshambuliaji wa Manchesater United Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la ushindi dakika za mwisho na kumpatia mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho kombe lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo kwa kuishinda Southampton.
Southampton walionyesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo lakini wakavunjwa moyo na uamuzi wa utata uliompa bao la ushindi raia huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 35.
Mshambuliaji wa Saints Manolo Gabbiadiani alifunga bao lililokataliwa kabla ya Manchester United kupata bao la pili kupitia Ibrahimovic kunako dakika 19 kabla ya Jesse Lingard kufunga ikiwa imesalia dakika saba mechi kukamilika.
Southampton ilifunga mabao yake mawili kupitia Gabbiadiani katika vipindi vyote viwili vya mechi.
Oriel Romeu alipiga mwamba wa goli kabla ya Ibrahimovic kufunga kupitia krosi iliopigwa na Anders Herrea dakika tatu kabla ya mechi kukamilika na hivyobasi kuipatia ushindi Manchester United.
0 Maoni:
Post a Comment