LA LIGA: REAL WATOKA NYUMA 2-0 NA KUSHINDA, SASA WAKO JUU YA BARCA KILELENI.

RONALDO AWEKA REKODI YA MATUTA LA LIGA!
Tokeo la picha la real madrid vs villarreal 2017

REAL MADRID Jana Usiku walitoka nyuma kwa Bao 2-0 na kuicharaza Villareal 3-2 Ugenini na kutwaa uongozi wa La Liga ambao mapema Jana ulishikiliwa na Barcelona waliowachapa Atletico Madrid 2-1 huko Vicente Calderon.

Matokeo hayo yamewapa uongozi Real wakiwa na Pointi 55 kwa Mechi 23 na Barca ni wa Pili wakiwa na Pointi 54 kwa Mechi 24.

Timu ya 3 ni Sevilla wenye Pointi 52 kwa Mechi 24.
Villareal walifunga Bao zao Dakika za 50 na 56 kupitia Trigueros Muñoz na Bakambu lakini Gareth Bale akaipa Bao Real Dakika ya 64.

Kisha Refa akaipa Real Penati baada ya Mchezaji wa Villareal Bruno kuunawa Mpira na Cristiano Ronaldo kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 74.

Bao la 3 na la ushindi kwa Real lilipachikwa Dakika ya 83 na Alvaro Morata alienzia Benchi Mechi hii.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
JE WAJUA?
  • Cristiano Ronaldo ndie sasa Mfungaji Bora wa Penati kwenye La Liga kwa kupachika Penati 57 baada ya Jana kufunga Bao la Pili kwenye Mechi na Villareal.
  • Kabla Mechi hiyo, Ronaldo alikuwa amefungana na Lejendari wa Real Hugo Sanchez baada ya Ronaldo kufunga Penati hapo Januari 15 walipofungwa 2-1 na Sevilla.



Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment