WIKIENDI
hii La Liga ina mpambano mkali huko Vicente Calderon Jijini Madrid,
Spain wakati Wenyeji Atletico Madrid wakiwakaribisha FC Barcelona hapo
Jumapili.
Siku hiyo hiyo, Vinara wa La Liga, Real Madrid, ambao wako Pointi 1 mbele ya Barca, wapo Ugenini kucheza na Villareal.
Mechi
ya Atletico na Barca itakuwa ni Mechi ya 300 kwa Kocha kutoka Argentina
Diego Simeone kuiongoza Atletico lakini amekuwa hana matokeo mazuri
dhidi ya Barca kwenye La Liga licha ya Msimu wa 2012/13 kutwaa Ubingwa
wa Ligi hiyo likiwa Taji lao la kwanza katika Miaka 18 na pia kumaliza
wa Miaka 10 wa Barca na Real kubadilishana Ubingwa.
Katika
Miaka 15 kabla ujio wa Simeone hapo 2011, Atletico walikuwa wametwaa
Makombe Mawili tu lakini tangu wakati huo Atletico sasa imetwaa Vikombe
Vitano.
Vikombe hivyo ni EUROPA LIGI, UEFA SUPER CUP, Copa del Rey na Spanish Super Cup.
Pia
Simeone aliongoza Atletico kuifunga Barca hapo Vicente Calderon mara 2
katika Misimu Mitatu iliyopita na kufika Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI.
Lakini kwenye La Liga, Atletico wamefungwa Mechi 16 na Barca.Chini ya Diego Simeone, Atletico Wameshinda Mechi 187, Sare 61 na Kufungwa 51 katika Mechi zake 299.
Hivi
sasa Barca wanaonyesha kuyumba kwani Wiki iliyopita walicharazwa 4-0 na
Paris Saint Germain kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na kisha kushinda kwa
mbinde Mechi ya La Liga na Leganes huku Bao lao la Pili likifungwa
Dakika ya 90 kwa Penati ya Lionel Messi.
Kwa
Atletico, wao wako kipindi murua kwani wameshinda Mechi 2 Ugenini 4-1
wakiichapa Sporting Gijon kwenye La Liga na kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI
kuicharaza Bayer Leverkusen 4-2.
LA LIGA
Ratiba:
Jumapili Februari 26
1400 RCD Espanyol v Osasuna
1815 Atletico de Madrid v FC Barcelona
2030 Athletic de Bilbao v Granada CF
2030 Sporting Gijon v Celta de Vigo
2245 Villarreal CF v Real Madrid CF
0 Maoni:
Post a Comment