Rais wa FIFA Gianni Infantino amezindua ujenzi wa Hoteli ya chama cha soka cha Rwanda kwa gharama za FIFA.
Bwana Infantino ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hoteli hiyo inayojengwa mjini Kigali karibu na uwanja wa taifa Amahoro.
FIFA
tayari imeshatoa kitita cha dolla za Marekani milioni 4,1 kwa ajili ya
ujenzi wa Hoteli hiyo huku zikiwa zimesalia dolla milioni 2.
Mwenyekiti
wa chama cha soka cha Rwanda FERWAFA Bwana Nzamwita De Gaule, amesema
Hoteli hiyo itatumiwa kupokea timu mbali mbali kutoka ng'ambo
zinazokwenda kucheza nchini Rwanda.
"Hii Hoteli itakuwa na vyumba 48 vikiwemo vyumba 4
vitakavyojengwa kwa ajili ya walemavu.itakuwa na uwezo wa kupokea timu
mbili za taifa kwa wakati mmoja au vilabu 3 kwa wakati mmoja".Amesema
mkuu wa chama cha soka cha Rwanda.
Amesisitiza mradi wa Hoteli
hiyo ulilenga kukiwezesha chama cha soka cha Rwanda kuwa na uwezo wa
kupata pesa za kuendeleza soka nchini Rwanda.
"Tumekuwa
tukigharamia kulipia hoteli timu zinazokuja kucheza hapa Rwanda katika
mashindano mbali mbali ,hata timu yetu ya taifa kuipeleka katika hoteli
nyingine ilikuwa gharama kubwa.Sasa mradi huu utatusaidia na kuturuhusu
kuingiza pesa za kuendeleza soka letu."
Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema aliidhinisha
kugharamia mradi wa ujenzi wa Hoteli hii kwa sababu aliutambua kama
mradi mzuri wa kusaidia chama cha soka cha Rwanda kwa sababu una malengo
mazuri ya kuendeleza soka ambayo pia ndiyo malengo yake.
FIFA
itakuwa na mkutano wa kamati tendaji mwezi wa 10 mwaka huu nje ya makao
yake mjini Zurich,na Rwanda tayari imekwishaomba kuwa mwenyeji wa
mkutano huo.Kuhusu hilo Rais wa FIFA amesema uwezekano upo:
"Mpango ndio huo,lakini bado tunalijadili hilo.Tunaitambua Rwanda kutakuwa na mazungumzo zaidi kuhusu hilo" amesema Infantino.
Akiwa
ziarani nchini Rwanda Rais huyo wa FIFA amechukua fursa ya kuangalia
mechi ya ligi kuu ya soka ya Rwanda baina ya Rayon Sports na Police FC
iliyoshuhudia sare ya kufungana magoli 2-2 kwenye uwanja wa taifa
Amahoro.
0 Maoni:
Post a Comment