Mkufunzi wa Manchester United Jose
Mourinho amewashutumu wachezaji wa Leicester kwa kuwa na ubinafsi wa
kumsaliti aliyekuwa mkufunzi wao Claudio Ranieri.
Mkufunzi huyo
alivaa kofia yenye nembo za CR akimuunga mkono Claudio Ranieri kabla ya
kuwashutumu wachezaji hao ambao wengi wao walisaini kandarasi mpya
baada ya kushinda taji la ligi.
Muorinho alifutwa kazi katika
mandhari kama hayo msimu uliopita kufuatia mgomo wa wachezaji lakini
akasema kuwa kisa alichofanyiwa kilikuwa kidogo sana ikilinganishwa na
vile Ranieri alivyofanyiwa.
''Nadhani msimu huu ulianza na ubinafsi mwingi wachezaji wakitaka kupewa mikataba mipya'' .
''Watu wakifikiria fedha zaidi wengine wakiamua kuondoka bila kujali ni nani aliyewafanya kufikia walivyo'' alisema Mourinho.
0 Maoni:
Post a Comment