SANCHEZ KUTIMKIA MADRID?
Mshambuliaji tegemeo wa timu ya Arsenal Alexis Sanchez ameiambia klabu yake
kuwa anatamani kujiunga na miamba ya soka ya Hispania Real Madrid.
Don Balon inaripoti kuwa Madrid pia wanataka kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Chile ambapo inasemekana Arsenal wanataka dau la paundi 85 milioni ila huenda likapungua endapo Alvaro Morata atajumuishwa katika dili hilo.
Sanchez hajasaini mkataba mpya kutokana na kutoridhika na uwezo wa timu hiyo katika kugombania mataji huku mashabiki wa nchi yake wakiandaa maandamano ili atimke kwa Washika bunduki hao.
SPALLETTI AMLILIA RANIERI
Kocha wa AS Roma Luciano Spalletti amehuzunishwa na kutimuliwa kwa kocha wa Leicester City Claudio Ranieri akisema kuwa soka halina shukrani kwani mkufunzi huyo alistahili kupewa shukrani.
“Hakuna shukrani juu ya kile alichokifanya Ranieri ameibadilisha timu na kuisaidia kutwaa taji mwaka mwaka jana klabu haitakiwi kumlaumu mtu bali kuchukua majukumu kwa kile kilichotokea” Spalletti alisema hayo baada ya mchezo wa Europa ligi dhidi ya Villareal.
Ranieri ametimuliwa miezi tisa baada ya kuipa taji la ligi kuu nchini Uingereza kufuatia matokeo mabaya kwenye ligi wakipata alama moja katika pointi 18.
BONUCCI AMUOMBA RADHI ALLEGRI
Beki wa Juventus Leonardo Bonucci amejumuishwa katika kikosi cha klabu hiyo
kitakachocheza na Empoli baada ya kumuomba radhi kocha wake Massimiliano
Allegri kufuatia kugombana nae.
Bonucci aliachwa nje ya kikosi cha klabu hiyo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Porto baada ya kutofautiana na Allegri katika mechi na Palermo ambayo waliibuka na ushindi.
“Bonucci atakuwepo katika kikosi dhidi ya Empoli ni mchezaji muhimu kwetu na ameomba radhi” alisema Allegri.
MATTHAUS ASEMA LEWANDOWSKI NI ZAIDI YA SUAREZ, BENZEMA, COSTA
Beki wa zamani wa klabu ya Bayern Munich Lothar Matthaus amesema mshambuliaji wa klabu hiyo Robert Lewandowski ni hatari zaid ya Karim Benzema, Luis Suarez na Diego Costa.
Beki huyo alisema Lewandowski yupo katika kiwango bora kwa sasa amefunga mabao 25 katika mechi 31 katika michuano yote barani Ulaya.
“Kwangu mimi Lewandowski ni mshambuliaji namba tisa mkali zaidi duniani akiwazidi Benzema, Suarez na Costa kwa maana anajua kufunga na ni mmaliziaji mzuri” Matthaus aliiambia Sport Bild.
LEICESTER WATOA ORODHA YA WAKUMRITHI RANIERI
Baada ya kupita masaa 24 tangu klabu ya Leicester City kumtimua aliyekuwa kocha wao Claudio Ranieri hatimaye timu imetoa orodha ya makocha ambao huenda mmoja wao akachukua mikoba ya Muitaliano huyo.
Muitaliano mwenzake Roberto Mancini anaongoza katika orodha hiyo huku makocha kama Guus Hidink, Frank De Boer na Nigel Pearson wakipewa nafasi ya kuongozi jahazi hilo.
Ranieri ametimuliwa klabuni hapo kufuatia matokeo mabaya katika ligi kuu nchini Uingereza licha ya kufanikiwa kuingia hatua ya 16 bora klabu bingwa barani Ulaya.
LACAZETTE KUMRITHI GRIEZMANN ATLETICO
Klabu ya Atletico Madrid imeanza kutafuta mbadala wa mshambuliaji Antoine Griezmann huku wakionyesha dalili za kukubali Mfaransa huyo kutimkia Manchester United.
Atletico imemuona mshambuliaji wa Olympique Lyon Alexandre Lacazette kuwa mbadala sahihi wa nyota huyo. Lacazette ana mkataba mrefu na klabu yake hivyo itawabidi Wahispaniola hao kuandaa ofa ya paundi 40 milioni mwezi Juni.
Lacazette amekuwa na msimu mzuri katika siku za karibuni huku akihusishwa na klabu kubwa barani Ulaya zikiwemo Real Madrid, Chelsea na Arsenal.
0 Maoni:
Post a Comment