FA CUP: ARSENAL YATINGA ROBO FAINALI.

Tokeo la picha la arsenal vs sutton fa image
Arsenal Jana Usiku ilifuzu Robo Fainali ya EMIRATES FA CUP baada ya kuifunga Timu ambayo haiko mfumo rasmi wa Ligi huko England Sutton United 2-0.

Kwenye Robo Fainali Arsenal itacheza na Timu nyingine ambayo nayo haiko mfumo rasmi wa Ligi huko England Lincoln City.

Bao za Arsenal hapo Jana wakicheza Ugenini zilifungwa Dakika za 26 na 55 na Martinez Lucas Perez na Theo Walcott.

JE WAJUA?
  • FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

  • Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.
  • Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
  • Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
  • Bingwa Mtetezi ni Manchester United.
###################################################
FA CUP - Robo Fainali.
DROO KAMILI:
Mechi hizi zitachezwa Wikiendi ya Machi 10 hadi 13.
Chelsea v Man United
Middlesbrough v Huddersfield au Man City
Tottenham v Millwall
Arsenal v Lincoln City

VIKOSI:

Sutton United: Worner, Amankwaah, Downer, Collins, Beckwith, Deacon, Bailey, Eastmond, May, Gomis, Biamou
Akiba: John, Hudson-Odoi, Fitchett, Spence, Monakana, Tubbs, Shaw.

Arsenal: Ospina; Gabriel, Mustafi, Holding, Monreal; Elneny, Xhaka; Lucas, Reine-Adelaide, Iwobi; Walcott
Akiba: Martinez, Debuchy, Mertesacker, Gibbs, Maitland-Niles, Oxlade-Chamberlain, Sanchez.

Tokeo la picha la Michael Oliver image
                  REFA: Michael Oliver.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment