Mshindi wa mara kumi na nne wa mchezo wa Golf Tiger Woods
amesema kamwe yeye hataendelea kujiona ni mchezaji mkubwa kwa sababu
ya kukabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi katika fani yake.
Woods
mwenye miaka 41, alitupwa nje ya mashindano ya Dubai Desert Classic
kabla ya duru ya pili ya mwezi huu kwa sababu ya maumivu, alitarajia
kurejea tena dimbani mwezi wa kumi na mbili baada ya kufanyiwa upasuaji.
Ameviambia
vyombo vya habari vya Dubai kuwa kwa muda mwingi kuwa kumekuwa na
changamoto nyingi hakuweza kufikiria kurejea tena na ilikuwa ni
vigumu.
Na kwa sasa Ana matumaini ya kushindana katika michuano ya Masters kuanzia mwezi April.
0 Maoni:
Post a Comment