Klabu ya soka ya Leiceister city hatimaye imeweza kulinda heshima
katika uwanja wake wa nyumbani wa king power kufuatia ushindi wa magoli
3-1 dhidi ya Derdy County katika michuano ya mwaka huu ya FA CUP ukiwa
ni mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kutinga Raundi ya 5 ya
michuano hiyo.
Hadi dakika 90 za mchezo zinamaliziaka timu hizi tayari zilikuwa zimefungana bao 1-1 na kulazimia kuongezwa muda wa ziada.
Leiceister
city ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Andy King ,na
baadaye Derdy County wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Abdoul Camara,
huku Onyinye Wilfredy Ndindi akiongeza bao la pili kwa upande wa
Leceister city katika dakika ya 94 muda wa nyongeza.
Dakika ya 114 Demaria Gray akapigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Derby County kwa kuandika bao la tatu na la mwisho.
Kwa matokeo hayo sasa Leiceister city watakutana na Milwall katika raundi ya tano wakiwa ugenini.
0 Maoni:
Post a Comment