LALLANA: UMAKINI NA UZOEFU NI CHANGAMOTO LIVERPOOL.

Tokeo la picha la adam lallana image
Kiungo wa klabu ya soka ya Liverpool Adam Lallana
Kiungo wa klabu ya soka ya Liverpool Adam Lallana amesema kuwa kukosekana kwa mambo muhimu ya ziada ya kiuzoefu katika timu yao wakiwa hawapo vyema ndio sababu na changamoto ya azma yao kutwaa Ubingwa wa England.

Kauli hiyo imefuatia baada ya hivi karibuni Liverpool kushindwa kufanya vizuri dhidi ya Hull City na kutupwa Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England, wakiwa alama 13 nyuma ya Vinara Chelsea.

Liverpool, chini ya Meneja Mjerumani Jürgen Klopp, hawajashinda hata Mechi 1 ya ligi kuu Mwaka huu 2017 na kutupwa nje ya 4 Bora kwa mara ya kwanza tangu Septemba 24.

Kabla ya Mechi na Hull city Liverpool, wakiwa nyumbani Anfield, walitoka Sare na Vinara Chelsea na hilo lilitegemewa kuwafanya wageuke na kuanza kupata ushindi lakini hali ikawa ni tofauti na mategemeo.

Kipigo toka kwa Hull kimeendeleza mwenendo wao wa kufungwa na Timu 'dhaifu' kama vile walivyofanywa Msimu huu na Timu zilizo Nafasi za 9 za mwisho ambazo ni Burnley, Bournemouth, Swansea City na hiyo Hull. Na Lallana amekiri kuwa kukosa uzoefu kunawaathiri.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment