Kocha wa mabingwa soka Tanzania bara Timu ya Yanga Mzambia George
Lwandamina ametamba kwamba mechi dhidi ya timu ya Ngaya Club ya
Comoro katika mchezo wa klabu bingwa afrika zitawapa taswira nzuri
kabla ya kuvaana na maasimu wao Timu ya Simba Februari 25, mwaka huu
katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Yanga inatarajia kuchuana na Simba Februari 25, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .
Kwa
sasa Yanga wapo kileleni mwa Ligi hiyo kwa alama 49, wakifuatiwa na
Simba yenye alama 48 baada ya timu zote kucheza michezo 21.
Mara
ya mwisho timu hizo zilikutana katika Nusu Fainali ya Kombe la
Mapinduzi Januari 10, mwaka huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar na Simba
ikashinda kwa penalty 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90
0 Maoni:
Post a Comment