Nahodha wa Bayern Munich Philipp
Lahm, aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani walipotwaa Kombe
la Dunia mwaka 2014, ametangaza kwamba atastaafu mwisho wa msimu.
Mchezaji
huyo wa miaka 33 ametangaza uamuzi huo baada ya Bayern kushinda mechi
ya hatua ya 16 bora katika michuano ya Kombe la Ujerumani dhidi ya
Wolfsburg.
Ilikuwa mechi yake ya 501 kwake kuchezea viongozi hao wa Bundesliga.
"Ninaweza
kuendelea na mtindo wangu wa uongozi, kujitolea kila siku, kila kipindi
cha mazoezi, hadi mwisho wa msimu. Ninaweza kuendelea kufanya hayo
msimu huu lakini si zaidi ya hapo," amesema.
Hii ina maana kwamba ataondoka klabu hiyo mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.
Amesema amekuwa akitafakari kuhusu uamuzi huo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Alicheza
mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wachezaji wakubwa Bayern mwaka
2002 na ameshinda mataji saba ya Bundesliga akiwa na klabu hiyo, pamoja
na Kombe la Ligi ya Klabu.
0 Maoni:
Post a Comment