Kocha
wa zamani wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema yupo tayari
kurejea kujihusisha na soka kwa mara nyingine baada ya kustaafu kwa muda
kwa kuomba akabidhiwe majukumu ya ukatibu mkuu wa Simba.
Awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Patrick Kahemele ambaye aliamua kujiuzulu na kurejea Azam TV wiki iliyopita.
Julio
aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba kwa nyakati tofauti alijiweka
pembeni kujihusisha na masuala ya soka na kuikacha timu yake ya Mwadui
baada ya kuchoshwa na maamuzi mabovu ya waamuzi wa ligi kuu.
Julio
amesema kuwa kwa upande wake hana wasiwasi endapo viongozi wa Simba
wakiongozwa na rais wake, Evans Aveva wakiamua kumpa nafasi hiyo kwani
anaamini ana uwezo wa kuongoza.
“Siyo
kama najipigia chapuo lakini kama viongozi wa Simba wakiamua kunipa
nafasi ya ukatibu sitaweza kukataa kwa sababu naipenda timu hiyo na kila
mmoja anajua na kama nikiwepo naamini nitaongezea kitu fulani na
kuifanya timu ipate matokeo mazuri.
“Uzuri
wangu kwangu kwamba sikufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na soka hivyo
hata nikirejea hakuna ambaye atashtuka na niwaahidi kwamba nitaitumikia
nafasi hiyo kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa kipindi kirefu,”
alisema Julio.
SOURCE: CHAMPIONI
0 Maoni:
Post a Comment