Kocha
wa muda wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kwa sasa kikosini kwake
hakimtegemei mchezaji mmoja kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye
uwezo unaofanana.
Cheche
ameyasema hayo baada ya kuwakosa nyota wake wanne kwenye mechi mbili
walizocheza ambazo waliweza kukusanya pointi nne kati ya sita.
Wachezaji
hao aliowakosa ni John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Stephane
Kingue na Shomari Kapombe ambao wanasumbuliwa na majeraha mbalimbali.
Hawa
walishindwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mamelod Sundowns
waliyotoka suluhu na mchezo wa Ligi Kuu Bara walioibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Ndanda.
Akizungumza na Championi Jumatano, Cheche alisema:
“Hapa hatumtegemei mchezaji mmoja, kama huyu akikosekana basi yupo mwingine ambaye naye anaweza kuziba pengo kiufasaha zaidi.
“Mechi
mbili tumecheza bila ya wachezaji wetu wanne ambao ni wa kikosi cha
kwanza, lakini matokeo tuliyoyapata si mabaya, tumeshinda na sare, hivyo
sina wasiwasi ikitokea wachezaji wangu wa kikosi cha kwanza wamepata
majeraha, wapo watakaokuja kucheza nafasi zao.”
0 Maoni:
Post a Comment