Straika
wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe ameshukuru kitendo cha
Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kurudishia namba yake ya jezi baada ya
kumpokonya katika michuano iliyopita ya Mabingwa Afrika.
Katika
michuano hiyo, Tambwe alijikuta ikilazimika kutumia jezi yenye namba 19
badala ya 17 kutokana na makosa yaliofanywa na uongozi wa Yanga wakati
ulipokuwa ukituma majina ya wachezaji wake watakaoiwakilisha timu hiyo
kwenye michuano hiyo.
Hata
baada ya Yanga kugundua kuwa ulikosea kutuma namba ya jezi ya Tambwe na
kuiomba Caf ilifanyie marekebisho suala hilo iligonga mwamba jambo
ambalo lilimfanya mchezaji huyo kulazimika kuitumia jezi namba 19 kwenye
michuano hiyo bila ya kutaka na kumuacha akitumia 17 katika michuano ya
Ligi Kuu Bara tu.
Tambwe alisema kuwa amefurahi sana kurudishwa namba yake hiyo ya jezi na Caf baada ya kuikosa msimu uliopita.
“Hakika
msimu uliopita nilipoteza amani baada ya kuikosa jezi yangu hiyo kwani
nimeizoea, hata hivyo kitendo cha Caf kunirudishia msimu huu kimenifanya
nijisikie vizuri sana,” alisema Tambwe.
0 Maoni:
Post a Comment