Manchester City wanamatumaini kuwa
kiungo wa mbele Gabriel Jesus, hakupata jeraha baya la mguu wakati wa
mechi yao waliyowashinda Bournemouth mabao 2-0.
Jesus mwenye umri
wa miaka 19 alifunga mabao katika mechi mbili za kwanza tangu ajiunge
City, lakini alicheza tu dakika 14 wakati wa mechi na Bournemouth
kufuatia jeraha. Man City watabainisha hali ya jereha lake leo.
Tunamatumaini kuwa halitakuwa tatizo kubwa, meneja wa City Pep Guardiola aliiambia BBC.
Jesus
ambaye alitokea Palmeiras mwezi Januari, alifunga mabao ya ushindi
wakati walipokutana na West Ham na baadaye Swansea na alikuwa mbioni
kuwa mchezaji wa tatu wa city baada ya Emmanuel Adebayor na Kevin de
Bruyne, waliofunga mabao wakati wa mechi zao tatu za kwanza mara baada
ya kujiunga na Man City.
0 Maoni:
Post a Comment