KIKOSI cha Yanga kimetua uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kikitokea nchini Comoro
walikopata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ngaya de Mbe.
Mashabiki wa timu hiyo wamewalipa vijana hao
ushindi wao kwa mapokezi ya nguvu yaliyoambatana na nyimbo na shangwe
zilizoonyesha wazi jinsi walivyofurahishwa na matokeo hayo.
Mashabiki hao walifika mbali pale walipoamua
kulisukuma kwa mikono basi lililowabeba wachezaji hivyo dereva kutolazimika
kuweka gia ili lisogee mbele.
Yanga sc wanafaida ya
ushindi mnono walioupata ugenini ni dhahiri sasa wanasubiri mshindi kati
ya Zanaco vs APR ya Rwanda ambao mchezo wao wa kwanza uliisha kwa sare
ya bila kufungana.
0 Maoni:
Post a Comment