MAN CITY YAPATA PIGO GABRIEL JESUS NJE MIEZI KADHAA.



Mshambuliaji Gabriel Jesus wa Manchester City amevunjika mfupa wa tano wa mguu maarufu kama metatarsal.

Jesus ambaye alionekana ni mkombozi wa Man City katika ushambulizi alivunjika katika dakika ya 14 ya mchezo dhidi ya Bournemouth ambao City walishinda kwa mabao 2-0.
 
Na sasa huenda akawa nje kwa Miezi kadhaa. City imethibitisha hilo lakini imeeleza anapaswa kuchunguzwa zaidi ili kupata undani.
 
Jesus, mwenye Miaka 19, aliumia Juzi Jumatatu Usiku City ilipoifunga Bournemouth 2-0 huko Vitality Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England. Jesus aliumia na kutolewa nje kwenye Dakika ya 15

Lakini tayari amepatiwa matibabu na inaonekana maendeleo ni mazuri.



TAKWIMU ZAKE PREMIER LEAGUE
Mechi 4  
Nafasi alizotengeneza 4 
Mashuti yaliolenga 4  
Mabao aliyofunga 3 
Pasi za mabao 1 


              
 
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment