Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo miwili tu. Michezo
ya kesho kwa mujibu wa Ratiba ya VPL ni kati ya Ndanda FC
itakayoikaribisha Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona
mjini Mtwara wakati Kagera Sugar ya Kagera itakuwa mgeni wa Tanzania
Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi nyingine zitachezwa
Februari 17, 18 na 19 kwa mujibu wa Ratiba ambayo nimeambatanisha hapo
chini.
SERENGETI BOYS KUTEMBELEA SOBER HOUSE
Timu
ya Taifa ya mpira wa miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya
miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Jumamosi tarehe 04 Machi, 2017, watatembelea
Kituo cha vijana wanaopatiwa matibabu baada ya kuathirika na dawa za
kulevya.
Kituo
hicho kinachoitwa Sober House kipo Bagamoyo mkoani Pwani. Ni kituo
maalumu kwa tiba ya vijana kinaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Life
and Hope Rehabilitation Centre chini ya Mkurugenzi, Al-Karim Bhanji.
Ikiwa
huko, vijana wa Serengeti Boys ambao kwa sasa wako kwenye kipindi cha
mabadiliko ya katika sayansi ya mwili hivyo itakuwa somo kubwa kwao
katika kujielimisha kuhusu mustakabali wa maisha yao.
Kwa
upande wa TFF kuwapeleka vijana hao huko ni utekelezaji Kanuni ya 36 (7)
ya Ligi Kuu ya Vodacom inayozungumza kukataa rushwa, madawa, ubaguzi,
fujo, kamari na mambo mengine ya hatari kwa mchezo wa mpira wa miguu.
PONGEZI LIPULI KUPANDA DARAJA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
ameuandikia barua uongozi wa Lipuli ya Iringa kwa mafanikio ya kupanda
daraja msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/18.
Lipuli
ya Iringa imepanda daraja baada ya kupita miaka 17 na Rais Malinzi
amesema katika barua yake hiyo kwenda kwa Katibu Mkuu wa Lipuli,
akisema: “Nitumie fursa hii kukupongeza wewe, uongozi wa klabu yako,
benchi la ufundi na wadau wote wa timu ya Lipuli kufuatia kupanda daraja
kwenda Ligi Kuu.
“Bila
shaka ni kazi kubwa imefanyika ikihusisha kujitolea kwa ari na mali
kuhakikisha mnafika hapa mlipo,” ilisema barua hiyo na kuongeza: “Rai
yangu kwenu ni kuongeza juhudi na kuendesha klabu kwa weledi mkubwa
zaidi ili muweze kuwa washindani wa kweli katika ligi.”
Lipuli
iliyokuwa kundi “A” imepanda daraja na kuzipiku timu za Kiluvya United
ya Pwani, Pamba ya Mwanza, African Sports ya Tanga, Polisi Dar, Ashanti
United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam.
SITA BORA LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA BARA 2016/2017
Baada
ya timu sita (6) kutinga hatua ya Sita Bora ya Ligi Kuu ya Wanawake ya
Shirilkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufahamika, ratiba rasmi ya
michuano hiyo, imetoka na inaonyesha kuwa hatua hiyo ya kutafuta bingwa
wa msimu, itaanza Februari 18, mwaka huu.
Timu
sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es
Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A”
wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma
na Panama ya Iringa.
Kwa
mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo
kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko
Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00
mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.
Ratiba
inaonesha kwamba siku ya Februari 18, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati
ya JKT Queens na Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na
mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.
Februari
20, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Panama saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi
na Fair Play.
Februari
22, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisterz na Marsh Academy saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na
JKT Queens.
Februari
24, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na JKT Queens saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Marsh
Academy na Mlandizi Queens.
Februari
26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Sisters saa 8.00
mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na
Marsh Academy.
Februari
28, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisters na Mlandizi Queens saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na
Fair Play.
Machi
2, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Acedemy na Fair Play saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi
na Panama.
Machi 3, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu saa 10.00 jioni ambako JKT Queens watamaliza na Sisterz.
SIMBA, AFRICAN LYON RAUNDI YA 6 AZAM SPORTS FEDERATION KUCHEZA ALHAMISI FEBRUARI 16
Raundi
ya Sita ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani
Azam Sports Federation Cup – 2016/17, itaanza Februari 16, 2017 badala
ya Februari 24, mwaka huu.
Mchezo
huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja
kabla ya kuendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne
kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu
utakaopigwa saa 1.00 jioni.
Michezo
hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya
Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.
Mechi
nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC
ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali
Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika
saa 1.00 usiku.
Jumapili
Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na
Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
MAYANGA AKABIDHI PROGRAMU TFF
Kocha
Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga
amekabidhi programu ya miezi sita kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi akianzia mechi ya
kirafiki za kimataifa kabla ya mechi za ushindani.
Mechi
hizo ni kwa za wiki kwa mujibu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) na kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) ambako kwa kuanzia tu, ataanza maandalizi ya mechi za wiki ya
FIFA ambazo zitachezwa kati ya Machi 21 na 29, mwaka huu.
TFF bado inaratibu michezo dhidi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro kwa maana ya wapinzani wao hapo baadaye.
Mwezi
Aprili, kati ya tarehe 20 hadi 22, 2017 kutakuwa na mechi za kufuzu kwa
michuano ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaokipiga Ligi ya Ndani (CHAN) ambako Taifa Stars itacheza
na Rwanda katika hatua za awali. Fainali za CHAN zitafanyika Kenya
mwakani.
Kwa
mujibu wa ratiba, Juni 6 hadi 13, mwaka huu kutakuwa na mechi za kufuzu
kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Lesotho
katika mchezo utakaofanyika hapa Tanzania.
Kwenye
AFCON Tanzania iko kundi “L” ambalo wapinzani wake wako Lesotho
watakaoanza kucheza nao hapa nyumani kabla ya huko mbele kucheza na
Uganda na Carpe Verde. Fainali za AFCON zinatarajiwa kufanyika Cameroon,
mwaka 2019.
IMETOLEWA NA TFF
0 Maoni:
Post a Comment