STAMFORD BRIDGE JUMAMOSI: CHELSEA Vs ARSENAL, WENGER JUKWAANI KWA MASHABIKI WA CHELSEA.

Picha inayohusiana

WAKATI Meneja wa Arsenal Arsene Wenger akiwa Jukwaani miongoni mwa Mashabiki wa Chelsea kushuhudia Arsenal ikiwavaa Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, Meneja wao Antonio Conte ameitaka Timu yake kutumia nafasi hii murua kupiga hatua kuelekea Ubingwa.
 
Wenger haruhusiwi kukaa Benchi la Ufundi la Timu yake kwa vile yupo Kifungoni na alipaswa kukaa Jukwaa la Wakurugenzi lakini muundo wa Stamford Bridge ni tofauti na akikaa huko atakuwa mbali na Benchi la Ufundi kwa vile liko upande wa pili wa Uwanja.

Ili kuwa karibu na Benchi, Wenger atalazimika kukaa pamoja na Washabiki wa Chelsea akiwekewa ulinzi mkali.
Kifungo cha Wenger hakimzuii kutoa maelekezo wakati wa Mechi.

Hivi sasa Chelsea wanaongoza EPL wakiwa Pointi 9 mbele huku Gemu zikibaki 15 na wakiifunga Arsenal, Timu ambayo iliifunga Chelsea 3-0 kwenye Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu huko Emirates.

Kipigo hicho kiliibadilisha Chelsea na Conte akaja na Mfumo mpya wa 3-4-3 wakicheza Mechi 17 za Ligo na kufungwa 1 tu.

Pia vita nyingine katika mechi hii ni kati ya DIEGO COSTA NA ALEXIS SANCHEZ katika kugombania nafasi ya kuongoza katika ufungaji bora wa EPL.
 Tokeo la picha la chelsea vs arsenal match preview image

Conte ameeleza: "Zipo 15 zimebaki na ni Pointi 45. Wao ni Timu nzuri inayoweza kupigania Ubingwa na usisahau kwao walitufunga 3-0!"

Aliongeza: "Lakini hii ni nafasi nzuri kwetu na sisi ni Timu tofauti.

Wakati Chelsea wanatinga Mechi hii wakitokea Anfield ambako Jumanne walitoka 1-1 na Liverpool, Arsenal wanatoka kwao Emirates walikodundwa 2-1 na Watford.

Hii ni Mechi ngumu kwa Arsenal kwani hawajashinda hapo Stamford Bridge tangu 2011.

Kipa wa Arsenal Petr Cech, ambae kabla alidakia Chelsea na kutwaa nao Ubingwa mara 4, ameelezea kipigo cha Watford ni pigo kubwa katika azma yao ya Ubingwa na kuitaka Timu yao kukaza Buti.

EPL – Ligi Kuu England Ratiba
***Saa za Bongo***

Jumamosi Februari 4
1530 Chelsea v Arsenal              
1800 Crystal Palace v Sunderland         
1800 Everton v Bournemouth              
1800 Hull City v Liverpool          
1800 Southampton v West Ham United          
1800 Watford v Burnley             
1800 West Bromwich Albion v Stoke City        
2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough 
              
Jumapili Februari 5
1630 Manchester City v Swansea City            
1900 Leicester City v Manchester United
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment